Tarimba, Sanga wazika tofauti zao sasa kusaidiana kuijenga Yanga
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Hatimaye ule mgogoro uliokuwepo kati ya kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mpito ya klabu hiyo Tarimba Abbas Tarimba wamezika tofauti zao leo na kuahidi kushirikiana pamoja ili kuijenga upya Yanga.
Wawili hao wamefikia maamuzi hayo baada ya tawi la Yanga, Viva Young International kuwaweka meza moja na hatimaye kufikia muafaka leo katika ofisi za Tarimba Abbas zilizopo Osterbay.
Tawi hilo lilianza kuzungumza na kila mmoja wao na hatimaye kuwakutanisha pamoja na kufikia muafaka, kuanzia sasa wawili hao wamekubaliana kufanya kazi pamoja na kuweka kando tofauti zao, Tarimba alijiuzuru nafasi yake ya kuongoza kamati ya mpito baada ya kuchukizwa na matamko ya Sanga aliyoyatoa katika mkutano wake na viongozi wa matawi