Makonda sasa kuitwa baba Keagan
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Poul Charles Makonda amemtunuku jina mwanaye la Keagan ili kudhihirisha napenzi yake kwa mkali wa soka Kevin Keagan.
Makonsa na mkewe wamebahatika kupata mtoto wa kiume baada ya miaka miwili ya ndoa yao, kwa furaha aliyonayo ya kupata mtoto, mheshimiwa Makonda aliandika katika ukurasa wake wa Instragram akielezea kumshukuru kwake mwenyezi Mungu.
Hata hivyo Makonda akaamua kumpachika jina mwanaye huyo wa kiume la Keagan ikidhihirisha mapenzi yake na mchezo wa soka, Mambo Uwanjani nayo inatoa salamu za pongezi kwa mkuu huyo wa mkoa kwa kupata mtoto