Yanga kujaribu tena kwa Gormahia

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc jioni ya leo wanapeperusha bendera ya nchi itakaposhuka uwanjani kuvaana na wenyeji wao timu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika kundi D.

Yanga ilisafiri juzi kuelekea mjini Nairobi ikiwakosa wachezaji wake wawili Hassan Kessy na Kelvin Yondani ambao wamegoma kusafiri wakishinikiza kupewa mikataba mipya.

Pia imewakosa wachezaji wake wapya watatu Mrisho Ngasa, Deus Kaseke na Heritier Makambo ambao usajili wao umechelewa kuwasilishwa CAF, katika mchezo wa leo Yanga inahitaji ushindi ama sare ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele ingawa haipewi nafasi ya kushinda kutokana na ubora ilionao Gormahia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons