Machapisho

KIPA MPYA AIBEBA LIVERPOOL IKISHINDA KWA MBINDE KOMBE LA LIGI

Picha
KIPA mpya wa Liverpool, Adam Bogdan usiku wa jana alikuwa shujaa Uwanja wa Anfield baada ya kuokoa penalti tatu na kuiwezesha timu hiyo kutinga Raundi ya Kombe la Ligi England.  Liverpool ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 na Carlisle ya Ligi Daraja la Nne England katika michuano ya Capital One. Mchezaji mwingine mpya, Danny Ings alianza kuifungia Liverpool kipindi cha kwanza kabla ya  Derek Asamoah kuisawazishia Carlisle na mchezo ukaenda kwenye dakika 30 za nyongeza. Penalti za Liverpool zilifungwa na Milner, Can na Ings wakati Lallana na Coutinho walikosa na za Carlisle zilifungwa na Dicker na Mcqueen huku Grainger, Joyce na Hery wakikosa. Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Bogdan, Clyne/Ibe dk86, Lovren, Milner, Firmino/Origi dk35, Moreno, Lallana, Can, Allen/Coutinho dk64, Ings na Skrtel. Carlisle: Gillespie, Miller, Raynes, Grainger, McQueen, Kennedy/Gillesphey dk73, Dicker, Joyce, Sweeney/Ibehre dk65, Hery na Asamoah/Gilliead dk64.

MAKALA: NI MECHI YA KUWANIA REKODI SIMBA NA YANGA

Picha
Mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi kwenye mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015/16. Timu hizi zilianza kupambana miaka mingi iliyopita, huku mechi zao zikivuta hisia za wapenzi wa soka nchini kabla na baada ya mechi. Pamoja na kwamba timu hizi zimekutana mara nyingi, lakini kuna baadhi ya mechi ambazo zilikuwa na matukio ambayo hayawezi kusahaulika kirahisi. Ni mechi ambazo zilikuwa na matukio mbalimbali ya kuhuzunisha, kuchekesha, kushangaza na nyingine kuweka rekodi ambazo hadi leo hazijafikiwa wala kuvunjwa. Yanga ilivyoifumua Simba 5-0 Achana na ile mechi ya 2012 Simba ilipoifunga Yanga mabao 5-0. Yanga iliwahi kufanya hivyo mwaka 1968. Ilikuwa Juni Mosi mwaka 1968,Yanga ilipoifumua Simba mabao 5-0. Magoli ya washindi yalifungwa na Maulidi Dilunga alipachika mabao mawili dakika ya 18 na 43, pia Selehe Zimbwe akifunga mawili dakika ya 54 na 89, Kitwana Manara akifunga goli moja dakika ya 8...

SHERMAN ANG'ARA 'BONDENI'

Picha
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman jana amecheza kwa dakika 63 timu yake mpya, Mpumalanga Black Aces ikiendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini. Aces imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini jana usiku, shukrani kwake mkongwe Collins Mbesuma aliyefunga mabao yote hayo dhidi ya Golden Arrows Uwanja wa King Zwelithini mjini Durban. Sherman alianza katika mchezo huo kabla ya kumpisha Aubrey Modiba dakika ya 63 wakati huo tayari Aces inaongoza 2-1. Deon Hotto alianza kuwafungia Arrows dakika ya 13 akimalizia pasi ya Gladwin Shitolo, lakini Mbesuma akasawazisha dakika ya 32 na kufunga la pili dakika ya 49. Sherman ametua Aces mwezi uliopita kutoka Yanga SC ambako alicheza kwa nusu msimu huu kabla ya kuamua kuondoka baada ya kuona mambo hayamuendi vizuri. Mechi nyingine za Ligi Kuu ya ABSA jana, Kaizer Chiefs imelazimishwa sare ya  1-1 University of Pretoria Uwanja wa FNB, bao lao likifungwa na Bernard Parker dakika ya 25 kabla ya  Te...

Van Gaal:Tutanyakua ubingwa wa ligi

Picha
Ushindi wa kilabu ya Manchester United dhidi ya Southampton ni dhihirisho tosha kwamba kilabu hiyo inaweza kunyakuwa taji la ligi kuu,amesema mkufunzi wake Louis Van Gaal. Kikosi hicho cha Van Gaal kilipata ushindi wa mabao 3-2 katika uwanja wa St Mary's siku ya jumapili huku mshambuliaji Anthony Martial mwenye umri wa miaka 19 akifunga mabao mawili. Ushindi huo umeipandisha kilabu ya Manchester United hadi nafasi ya pili nyuma ya Manchester City iliopoteza mabao 2-1 nyumbani dhidi ya West Ham siku ya jumamosi.''Tumeonyesha kwamba tunaweza kupigania taji hili'',Van Gaal alisema. Huwezi kutarajia taji kama hili kupitia timu iliopo katika awamu ya mpito,lakini iwapo tuko karibu kufanya hivyo basi tutalinyakuwa''. Van Gaal alipongeza uwezo wa Martial ,aliyefunga mabao matatu kufikia sasa kwa kujaribu mara tatu tangu alipowasili katika kilabu hiyo kupitia uhamisho wa kitita cha pauni milioni 36 kutoka Monaco.

TENGA AJIWEKA KANDO CECAFA

Picha
Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) linatarajia kupata mwenyekiti mpya atakayeliongoza shirikisho hilo katika uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethiopia imeelezwa. Hata hivyo,  Tenga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Rais wa zamani wa (TFF) bado hajaweka wazi kama atatetea nafasi hiyo katika uchaguzi ujao. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema kuwa mwenyekiti wa sasa, Leodegar Tenga, kutoka Tanzania anamaliza muda wake wa miaka minne wa kulitumikia shirikisho hilo tangu alipochaguliwa mwaka 2011 jijini Dar es Salaam. Musonye alisema kuwa tayari nchi wanachama wa Cecafa wanafahamu taarifa za uchaguzi huo ambao utafanyika kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Chalenji ambayo mwaka huu yatafanyika Ethiopia.

KUELEKEA MPAMBANO WA WATANI, YANGA WAINGIWA MCHECHETO NA HATI TRICK YA KIIZA 'DIEGO'

Picha
HAT TRICK ya kwanza ya msimu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imetoka kwa mshambuliaji Mganda, Hamisi Friday Kiiza maarufu kama Diego. Kiiza alifunga mabao matatu jana Simba SC ikishinda 3-1 dhidi ya timu ngumu, Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Na sasa Simba SC inakwenda kambini Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC wikiendi hii hapo hapo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tangu jana mashabiki wa Yanga SC wameanza kumuhofia Kiiza baada ya kuona na kusikia habari zake dhidi ya Kagera Sugar, hususan wakikumbuka alikuwa mchezaji wao. Kiiza aliichezea Yanga SC kwa miaka minne kabla ya kutemwa mwaka jana na kocha Mbrazil, Marcio Maximo ambaye alifukuzwa mwaka huo huo, nafasi yake ikichukuliwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm. Mashabiki wa Yanga SC hawakuridhishwa na kitendo cha kuachwa kwa Kiiza, lakini waliamua kukubali yaishe na mchezaji huyo akarejea kwao Uganda kupumzika.

SHAW WA MAN UNITED KUPIGWA KISU

Picha
Mlinzi wa kushoto wa Man United Luke Shaw atafanyiwa upasuaji wa pili leo katika mguu wake uliovunjika. Shaw yuko katika hospital ya St Anna Ziekenhuis alikopelekwa mara baada ya kuvunjika mguu katika mchezo wa ligi ya mabigwa dhidi ya PSV. Nyota huyu aliumizwa na beki Hector Moreno dakika ya 15 ya mchezo, familia ya mchezaji huyo imekwenda Uholanzi kumuangalia chipukizi huyo. Beki huyu kisiki wa upande wa kushoto ataukosa msimu mzima wa ligi na anatarajiwa kurejea uwanja tena mwezi Machi mwakani.