TENGA AJIWEKA KANDO CECAFA

Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) linatarajia kupata mwenyekiti mpya atakayeliongoza shirikisho hilo katika uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethiopia imeelezwa.

Hata hivyo,  Tenga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Rais wa zamani wa (TFF) bado hajaweka wazi kama atatetea nafasi hiyo katika uchaguzi ujao.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema kuwa mwenyekiti wa sasa, Leodegar Tenga, kutoka Tanzania anamaliza muda wake wa miaka minne wa kulitumikia shirikisho hilo tangu alipochaguliwa mwaka 2011 jijini Dar es Salaam. Musonye alisema kuwa tayari nchi wanachama wa Cecafa wanafahamu taarifa za uchaguzi huo ambao utafanyika kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Chalenji ambayo mwaka huu yatafanyika Ethiopia.


“Tutakuwa na mkutano mkuu kabla ya kuanza kwa mashindano na tutafanya na uchaguzi wa kupata mwenyekiti,” alisema Musonye ambaye ni Mkenya.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA