KIPA MPYA AIBEBA LIVERPOOL IKISHINDA KWA MBINDE KOMBE LA LIGI

KIPA mpya wa Liverpool, Adam Bogdan usiku wa jana alikuwa shujaa Uwanja wa Anfield baada ya kuokoa penalti tatu na kuiwezesha timu hiyo kutinga Raundi ya Kombe la Ligi England. 
Liverpool ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 na Carlisle ya Ligi Daraja la Nne England katika michuano ya Capital One.

Mchezaji mwingine mpya, Danny Ings alianza kuifungia Liverpool kipindi cha kwanza kabla ya  Derek Asamoah kuisawazishia Carlisle na mchezo ukaenda kwenye dakika 30 za nyongeza.

Penalti za Liverpool zilifungwa na Milner, Can na Ings wakati Lallana na Coutinho walikosa na za Carlisle zilifungwa na Dicker na Mcqueen huku Grainger, Joyce na Hery wakikosa.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Bogdan, Clyne/Ibe dk86, Lovren, Milner, Firmino/Origi dk35, Moreno, Lallana, Can, Allen/Coutinho dk64, Ings na Skrtel.

Carlisle: Gillespie, Miller, Raynes, Grainger, McQueen, Kennedy/Gillesphey dk73, Dicker, Joyce, Sweeney/Ibehre dk65, Hery na Asamoah/Gilliead dk64.


MECHI NYINGINE ZA JUZI NA JANA.

Manchester United imeshinda 3-0 dhidi ya Ipswich Town, mabao ya Wayne Rooney dakika ya 23, Andreas Pereira dakika ya 60 na Anthony Martial dakika ya 90+2 Uwanja wa Old Trafford, Newcastle United imefungwa 1-0 nyumbani na  Sheffield Wednesday bao pekee la Lewis McGugan Uwanja wa St. James' Park.

Arsenal imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane, mabao yake yakifungwa na Mathieu Flamini dakika ya 26 na 78, huku pia Calum Chambers akijifunga dakika ya 56 kuipa Spurs bao moja.

Chelsea pia imeshinda 4-1 ugenini, mabao yake yakifungwa na Ramires Santos do Nascimento dakika ya 10, Loic Remy dakika ya 41, Robert Kenedy Nunes do Nascimento dakika ya 52 na Pedro Rodriguez Ledesma dakika ya 90+2 Uwanja wa Bescot, huku bao pekee la wenyeji likifungwa na James O'Connor dakika ya 46).

Southampton imeifumua 6-0 MK Dons, mabao yake yakifungwa na Jay Rodriguez dakika ya tano na 48 kwa penalti, Sadio Mane dakika ya 10 na 25 na Shane Long dakika ya 68 na 75, wakati Everton pia imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Reading mabao yake yakifungwa na Ross Barkley dakika ya 62 na Gerard Deulofeu dakika ya 73, huku bao la wenyeji likifungwa na  Nick Blackman dakika ya 36 Uwanja wa Madejski.

Norwich City imeshinda 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion, mabao ya Matthew Jarvis dakika ya 62, Kyle Lafferty dakika ya 85 na Sebastien Pocognoli aliyejifunga dakika ya 90 Uwanja wa Carrow Road, Crystal Palace imeshinda 4-1 dhidi ya Charlton Athletic mabao yake yakifungwa na Fraizer Campbell dakika ya 51, Dwight Gayle matatu, mawili kwa penalti dakika ya 59 na 74 na lingine dakika ya 86, huku Mahamadou-Naby Sarr akifunga bao pekee la wapinzani dakika ya 65 Uwanja wa Selhurst Park.

Juzi Stoke City iliifunga 1-0 Fulham bao pekee la Peter Crouch dakika ya 33 Uwanja wa Craven Cottage, Hull City iliifunga 1-0 Swansea City bao pekee la David Meyler dakika ya 41 Uwanja wa KC.

Manchester City iliichapa 4-1 Sunderland mabao yake yakifungwa na Sergio Aguero kwa penalti dakika ya tisa, Kevin De Bruyne dakika ya 25, Vito Mannone (aliyejifunhga dakika ya 33 na Raheem Sterling dakika ya 36 Uwanja wa Light wakati Aston Villa iliifunga  1-0 Birmingham City bao pekee la Rudy Gestede dakika ya 62 Uwanja wa 
Villa Park.

Leicester City imeshinda 2-1 dhidi ya West Ham United, Bournemouth imeitoa Preston North End kwa penalti 3-2 baada ye sare 2-2, Middlesbrough imeifunga 3-0 Wolverhampton Wanderers mabao ya Albert Adomah dakika ya 37 na 64 na Diego Fabbrini dakika ya 57 Uwanja wa Riverside.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA