Van Gaal:Tutanyakua ubingwa wa ligi
Kikosi hicho cha Van Gaal kilipata ushindi wa mabao 3-2 katika uwanja wa St Mary's siku ya jumapili huku mshambuliaji Anthony Martial mwenye umri wa miaka 19 akifunga mabao mawili.
Ushindi huo umeipandisha kilabu ya Manchester United hadi nafasi ya pili nyuma ya Manchester City iliopoteza mabao 2-1 nyumbani dhidi ya West Ham siku ya jumamosi.''Tumeonyesha kwamba tunaweza kupigania taji hili'',Van Gaal alisema.
Huwezi kutarajia taji kama hili kupitia timu iliopo katika awamu ya mpito,lakini iwapo tuko karibu kufanya hivyo basi tutalinyakuwa''.
Van Gaal alipongeza uwezo wa Martial ,aliyefunga mabao matatu kufikia sasa kwa kujaribu mara tatu tangu alipowasili katika kilabu hiyo kupitia uhamisho wa kitita cha pauni milioni 36 kutoka Monaco.