Harusi ya mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi imeacha historia nchini Uganda akitumia dola 80,000 ( Sh 160,000 Mil ) kwa ajiri ya kuifanikisha iliyofanyika Jumamosi jijini Kampala. Kiasi hicho kinatosha kabisa kukamilisha usajili wa timu zisizopungua tatu za Ligi Kuu Bara, lakini yeye alitumia fedha hizo kwa ajili ya sherehe, huku Gazeti hili lilikuwa Uganda na kushuhudia kila kitu kilivyokuwa kinaendelea wakati Okwi akimuoa Florence Nakalega. Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza na Nabisubi Julian ndiyo walikuwa wasimamizi wao wa harusi hiyo, ilifungwa katika kanisa la Miracle Centre Cathedral lililopo Lubaga, Kampala.