Blatter: Sikujiuzulu kama rais wa FIFA


Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amekariri kuwa hakujiuzulu kama rais wa shirikisho hilo.

Kiongozi huyo mswissi mwenye mri wa miaka 79 alikuwa amedhaniwa kujiondoa madarakani juni tarehe 2 kufuatia kashfa kubwa ya ufisadi ulaji rushwa na matumizi mabaya ya madaraka iliyokumba shirikisho lake lakini sasa anaonesha dalili za kubadili mtazamo huo.

Blatter ambaye ameiongoza FIFA kwa miaka 17 alikuwa ametangaza kuwa atajiondoa mbele ya kamati kuu ili kufanyike uchunguzi wa kina katika FIFA lakini sasa ameikumbusha jarida moja la uswisi BLICK kuwa yeye ndiye rais wa FIFA na kuwa aliweka hatima yake mikononi mwa kamati kuu ya shirikisho katika mkutano wa dharura.


Hakuna mipango ya Blatter kuelekea Canada kwa Fainali ya kombe la Dunia la wanawake

Blatter anadhaniwa kuwa anafikiria kuwania tena uongozi wa shirikisho hilo.

Tuhuma za udhabirifu wa fedha ufisadi na ulaji rushwa ulianza katika ileile wiki ambayo Blatter alichaguliwa ikiendeshwa na Marekani.

Lakini punde baada ya uchaguzi utawala nchini Uswisi nao ukaanzisha uchunguzi sambamba wa ulaji rushwa na ufisadi dhidi ya maafisa wakuu katika shirikisho la soka duniani FIFA.

Blatter agoma kujiuzuru FIFA

Blatter alitangaza kuwa anajiondoa uongozini ili kuruhusu uchunguzi ufanyike siku nne tu baada ya kuchaguliwa upya kwa hatamu ya uongozi wa FIFA.

Kufuatia uchunguzi unaoendelea hakuna mipango na dalili zozote kuwa Blatter ama katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke atakuwa mjini Ontario Canada katika fainali ya kombe la dunia kwa wanawake.

Kwa kawaida Blatter angekuwa huko ilikutoa zawadi ya kombe la dunia kwa timu itakayoibuka mshindi lakini hadi kufikia sasa hakuna mipango yoyote ya ziara hiyo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA