UKATA WAMKWAMISHA MKOLA MAN KUTENGENEZA VIDEO YA MALAVIDAVI TIME

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Mkola Man anayewakilisha kundi la Sakainge lenye maskani yake Hale mkoani Tanga ameelezea masikitiko yake ya kushindwa kutoa video ya wimbo wake mkali wa 'Malavidavi Time'.

Mkola Man amesema kuwa ukata mkubwa uliomkumba ndio chanzo cha yeye kushindwa kutengeneza video ya wimbo wake wa 'Malavidavi time' ambao amemshirikisha mkali mwenzake kutoka kundi hilo hilo la Sakainge Yusa G.

Akizungumza na gazeti hili, Mkola Man amesema kwa sasa hana fedha za kuweza kutengeneza video hasa baada ya kuachishwa kazi, hivyo anawaomba wafadhili wajitokeze kumsaidia ili aweze kutengeneza video ya wimbo huo pamoja na kuandaa kazi mpya.

'Muziki ni ajira tosha, ila kwa sasa sina kitu zamani nilikuwa
najitegemea mwenyewe kwa sababu nilikuwa na sehemu ya kujipatia chochote lakini kwa sasa niko juu ya mawe hivyo naomba sapota yenu Wana-Tanga au Watanzania kwa ujumla', alisema msanii huyo aliyeanza kutamba na wimbo wake Mr Mapesa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA