Adebayor asema yuko tayari kuchezea Togo

Emmanuel Adebayor

Emmanuel Adebayor amemaliza kimya chake na kudai kuwa yuko tayari kuchezea Togo mechi ya kufuzu kwa Afcon dhidi ya Liberia Jumapili.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Togo pamoja na wenzake wawili walikuwa wamekataa kujiunga na timu ya taifa iliyoitwa na kocha mpya Tom Saintfiet kwa maandalizi ya mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika bila kutoa sababu zozote.
 
Na straika huyo aliyepewa likizo na klabu yake ya Uingereza Tottenham ili akatatue matatizo ya kifamilia na kiakili kabla ya msimu kumalizika, amedokeza kuwa bado anajiandaa baada ya kutazama mechi ya kirafiki ambayo Togo walilazwa 0-1 na Ghana uwanja wa Accra Sports Stadium Jumatatu.

“Bila shaka nimekuwa nikijiandaa kuwa sawa kucheza soka tena kwa sababu umekuwa muda mrefu sana tangu nicheze dakika 90 za soka,” fowadi huyo lalisema alipoulizwa ni kwa nini hakuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa uwanjani.


“Kuwa hapa hata kutazama mechi ni maridadi zaidi kwangu. Ninataka tu kurudi nyumbani na kuandaa mwili wangi kwa mechi ya wikendi [dhidi ya Liberia],” Adebayor akaongeza.

Kwake kuruhusiwa na kocha wao mpya kutoka Ubelgiji kujiunga na kambi sasa huenda likawa suala jingine kwani mdosi huyo wa zamani wa Malawi alikuwa amesema kwenye kikao na wanahabari baada ya mechi kwamba alilazimika kuchukua wachezaji waliojitokeza kuchezea taifa.

“Siwezi kumfuta au kumtaja mtu kwenye kikosi changu ilhali hata sijamuona kambini; hajafanya mazoezi na hajasema lolote kuhusu kushindwa kwake kujiunga na wenzake kambini,” akasema Saintfiet.
Togo watakaribisha nyumbani Liberia mjini Lome Jumapili alasiri.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA