SIMBA YATAMBULISHA KOCHA MPYA LEO, NI YULE ALIYEWAHI KUCHEZA LIGI YA UINGEREZA

Timu ya Simba imeingia makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja na kocha raia wa Uingereza, Dylan Kerr ya kukinoa kikosi hicho kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo, atatua kukinoa kikosi hicho ili kurithi kibarua cha Mserbia, Goran Kopunivoc aliyemaliza mkataba wa kukinoa kikosi hicho mwishoni mwa msimu uliopita wa ligi kuu.

Rais wa timu hiyo, Evans Aveva alisema kuwa kocha huyo anatarajiwa kutua nchini wiki hii tayari kwa kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho.

Avea alisema, kocha huyo mara ya kutua nchini atazungumza na Waandishi wa habari na Jumatatu ya wiki ijayo ataanza kibarua rasmi cha kukinoa kikosi hicho chini ya kocha msaidizi, Selemani Matola.


“Tumeingia makubaliano mazuri na kocha wetu mpya, Kerr tayari kwa kuanza kibarua cha kukinos chetu kwenye msimu ujao, hiyo ni baada ya kufikia muafaka kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

“Kocha huyo anatarajiwa kutua nchini wiki hii na Jumatatu ijayo ataanza mazoezi ya pamoja ya kuifundisha timu yetu tayari kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu.
“Pia ningependa kumtangaza kocha wetu mpya wa makipa mpya raia wa Kenya, Abdul Idd Salim ambaye ataanza kibarua cha kukinoa kikosi hichi,”alisema Aveva.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA