AZAM FC WAENDELEA KUSISITIZA MESSI WATAMCHUKUA.

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Azam FC Idrisa Nassor ameendelea kusisitiza kuwa watamchukua kiungo mshambuliaji wa Simba Ramadhan Singano 'Messi' aliye katika matatizo ya kimkataba.

Juzi klabu ya Simba ilifanya kikao chake na kuamua kukaidi agizo la TFF na kuendelea kuutambua mkataba wao na Messi unaokwisha julai 16 2016, lakini Azam inaamini itafanikiwa kumnasa Messi ambae kwa sasa yuko huru kufuatia mkataba wake na Simba kufutwa na TFF.

Akizungumza jana, Nassor amesema klabu yake inatamani kuwa na mchezaji Ramadhan Singano kwani ni mmoja kati ya viungo wa pembeni wanaofanya vizuri kwa sasa.


'Nakwambia lazima tumchukue Singano', alisema Nassor kwa kujiamini kabisa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI