KAMARA AFELI MAJARIBIO YANGA
Kiungo mpya wa Yanga, Msierra Leone Lansana Kamara amepewa mtihani mwingine na kocha Hans Pluijm akitakiwa kuhakikisha anajua kupiga mashuti ili kusajiliwa.
Udhaifu wa kiungo huyo ulionekana pale kocha Hans Pluijm alipowapa zoezi maalumu kupima ufanisi wao kwenye upigaji mashuti, ambalo kiungo huyo mkabaji hakulimudu ipasavyo.
Katika zoezi hilo, Pluijm alimtaka kila mchezaji kupiga mashuti 12 kuelekea kwenye lango ambalo lilikuwa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyekuwa amesimama.
Kiungo Kamara katika mashuti hayo alifanikiwa kupiga sita tu yaliyolenga langoni, huku mengine yakishindwa kulenga lango kwa kupaa na kutoka nje jambo lililoanza kuibua hofu kwa kundi kubwa la mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwenye Uwanja wa Karume eneo ambalo mazoezi hayo yalikuwa yakifanyika.
Katika mashuti sita ambayo yalilenga golini, Kamara alifunga mawili tu huku mengine manne yakiishia mikononi mwa kipa Barthez, ambaye alionyesha ustadi mkubwa wa kuokoa michomo iliyoelekezwa kwake.
Aliyekuwa kivutio katika zoezi hilo alikuwa ni mshambuliaji mpya wa Yanga, Jofrey Mwashiuya, ambaye alifanikiwa kufunga mashuti tisa, huku mengine matatu yakigonga mwamba.
Kamara aliliambia gazeti hili kwamba amekutana na Pluijm mara baada ya mazoezi ya jana asubuhi na kumueleza kuvutiwa na kila kitu anachofanya ndani ya uwanja ingawa alitaka aimarishe uwezo wa kupiga mashuti makali.
“Kocha amekubali kiwango changu na mazoezi mengi anayotupa ameniambia kuwa nafanya vizuri na niongeze juhudi.
“Lakini amesifu ninavyojitahidi kupiga mashuti makali, ila ameniambia kuwa mengi yanatakiwa kulenga lango nilifanyie kazi hilo taratibu nafikiri nitalifanyia kazi hilo taratibu.”
Kocha Pluijm ameridhika na jitihada za mchezaji huyo anazozionyesha mazoezini na kusema kwamba mazoezini ameridhika naye, lakini hawezi kufanya uamuzi wa mwisho hadi ampe mechi moja kwani wachezaji walioko mazoezini Yanga kwa sasa ni wachache.
“Huwezi kupata kipimo kizuri hapa mazoezini, nafikiri tunatakiwa kuwa na subira kwanza, nataka kumpa mechi moja ili nijue uwezo wake,” alisema Pluijm.