Recho atikisa 'Yuleyule ya PNC

Na Fikiri Salum

WIMBO mpya wa mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Panclas Ndaki Charles maarufu PNC uitwao 'Yuleyule' ambao tayari umeanza kukubalika kupitia vituo mbalimbali vya redio na runinga umeweza kumuibua video Queen mpya Rachel Njingo 'Recho',

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni PNC amesema video ya wimbo wake huo umeweza kumrudisha tena kwenye chati yake, PNC amesisitiza kuwa Recho ni bonge la video Queen na ameutendea haki wimbo huo.

'Sikutegemea kama wimbo wangu ungeweza kukubalika kiasi hicho lakini kila anayeutazama kupitia televisheni au mitandao ya kijamii hakusita kunipongeza', alisema PNC ambaye aliibukia mkoani Mwanza kabla hajajiunga na kundi la Tip top Connection lenye maskani yake Manzese Dar es Salaam.

Aidha msanii huyo amedai anatarajia kuanza ziara za mikoani kwa lengo la kuutambulisha wimbo wake huo lakini pia atapeleka zawadi kwa mashabiki wake ambao walimmiss
sana.PNC ambaye amejitoa kwa aliyekuwa mkurugenzi wake Ustaadh Juma na Musoma huku sababu za kujitoa kwake hazikuwekwa wazi, msanii huyo anaamini wimbo wa 'Yule yule' utafanya vizuri na kumweka katika matawi ya juu kama ilivyokuwa zamani alipatamba na wimbo wa 'Mbona' aliomshirikisha Mr Blue.




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA