Arsenal wamnunua chipukizi nyota wa Romania



Nahodha wa timu ya taifa ya Romania ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16 Vlad Dragomir amekataa ofa kutoka kwa mabingwa wa ligi ya kwao nyumbani Steaua Bucharest pamoja na timu kadha za ugenini na kuamua kujiunga na Arsenal kutoka ACS Poli Timisoara.

"Nina furaha na natumai sitamvunja moyo mtu yeyote,” kiungo huyo wa kati, aliyetia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza, aliambia vyombo vya habari Romania Jumatano.
“Ofa ya Arsenal ilinipendeza zaidi, nilihisi kwamba huko ndiko nafaa kwenda.”

Dragomir ndiye tineja wa pili kutoka Romania kujiunga na Ligi Kuu ya Uingereza mwezi huu baada ya Cristian Manea,
18, kujiunga na Chelsea akitokea FC Viitorul Constanta.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA