SIMBA YAJIAPIZA KUIBOMOA NDANDA LEO
MABINGWA wa soka wa kombe la Mapinuduzi Simba SC leo jioni inashuka kwenye uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara kukabiliana vikali na wenyeji wao Ndanda FC 'wana kuchele' timu ambayo imeipania vilivyo Simba. Uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Humphrey Nyosia umetamba kuwa ni lazima Simba iifunge Ndanda lakini kuhusu idadi ya magoli hiyo itajulikana uwanjani, akiongea na mtandao huu leo, Nyosia amesema kikosi cha Simba kimeimarika na kinaweza kushinda katika mchezo huo kwani wapinzani wao hawana ubavu hata kidogo.