KASEJA AWAAMBIA YANGA MSINITANIE MIMI BADO JANGWANI.

Mlinda mlango Juma Kaseja ameshtushwa na habari za kutimuliwa kwake na Yanga na kudai yeye hatambui maamuzi hayo kwani yametolewa nje ya muda muafaka wa usajili pili hajapewa barua ya kufukuzwa kwake.

Kaseja amesema yeye bado mchezaji halali wa Yanga na hatambui suala la kutimuliwa kwake.

Juzi uongozi wa Yanga ulitangaza kuachana na mlinda mlango Juma Kaseja kwa madai hajaripoti kwenye kituo chake cha kazi kwa muda mrefu na hajulikani halipo.


Kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga Jerry Muro amesema Yanga imeamua kuachana na Kaseja kwakuwa alikuwa mzigo kwao.

Kaseja aliingia matatizoni na klabu yake akiidai fedha zake za usajili zilizosalia ambazo ni mil 20, lakini uongozi wa Yanga ulimalizana naye kwa kumwekea ktk akaunti yake fedha hizo.

Kaseja aliendelea kulumbana na Yanga safari hiyo akilalamikia kitendo cha kuwekwa benchi na kudai wamekiuka mkataba waliokubaliana ambao ulikuwa unasema atakuwa kipa wa kwanza.

Lakini uongozi wa Yanga umekiuka masharti ya mkataba na kumwambia mwenye suala ya kuamua nani awe kipa wa kwanza ni mwalimu kitendo kilichopelekea yeye kusugua benchi karibu mechi zote ilizocheza Yanga zikiwemo za kirafiki.

Juzi uongozi wa Yanga ulitangaza kuachana naye na kuna mipango ya kutaka kumfungulia kesi ya kudai fidia kwa madai kuwa Kaseja amevunja mkataba kwa kutoweka kwenye eneo lake la kazi jambo ambalo Kaseja anapinga na kusema yeye anatambua ni mchezaji halali wa Yanga na walka hajapewa barua ya kuachwa na akipewa atazungumza na waandishi wa habari

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA