SIMBA KUVAANA NA TAIFA JANG'OMBE ILIYOSHINDA KWA SHILINGI
Wapinzani wa Simba katika hatua ya robo-fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani hapa wamepatikana kwa kurusha shilingi baada ya timu mbili za Kundi A, Polisi na Taifa ya Jang'ombe kumaliza katika nafasi moja.
Polisi, wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu, na Taifa ya Jang'ombe jana walimaliza mechi zao za hatua ya makundi wakitoka suluhu kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung visiwani hapa.
Matokeo hayo yaliwafanya wote wamalize nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Yanga wakiwa wamefanana kwa kila kitu baada ya wote kufungwa 4-0 dhidi ya Yanga kisha wote kuifunga Shaba FC ya Pemba bao 1-0.
Baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu hizo jana, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na Kamati ya Mashindano hayo walikutana na kuamua kurusha sarafu kwenye Uwanja wa Amaan kabla ya mechi ya Yanga dhidi ya Shaba FC saa mbili usiku jana.
Kinara wa Kundi C, Simba anakutana na 'best looser 2', (Polisi/Taifa) kwenye Uwanja wa Amaan leo.
GORAN AIPONDA SIMBA
Baada ya kuvuka kiunzi kwa JKU, Simba imefanikiwa kukwepa kukutana na timu ngumu za Azam FC na KCCA FC ya Uganda katika hatua ya robo-fainali ya michuano hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa leo.
Kikiwa na kocha mkuu mpya, Goran Kopunovic, kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU katika mechi kali ya mwisho ya Kundi C iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, mechi iliyompa ushindi wa pili mfululizo Mserbia huyo katika mechi mbili alizoiongoza timu hiyo tangu asaini mkataba wa miezi sita siku ya mwaka mpya.
Ushindi huo pia umeifanya Simba imalize kileleni mwa msimamo wa Kundi C ikiwa na pointi sita, moja juu ya Mtibwa Sugar walioko nafasi ya pili, hivyo kukwepa kukutana na timu ngumu za Kundi B, KCCA na Azam FC katika hatua inayoanza leo ya robo-fainali.
Goli lililoipeleka Simba fainali lilifungwa na winga Ramadhan Singano 'Messi' dakika nne kabla ya robo saa ya mchezo akiitendea haki kwa kupiga shuti kali la mguu wa kushoto pasi ya 'kuchopu' ya kiungo Said Ndemla baada ya kazi nzuri ya mshambuliaji Mganda Sserunkuma aliyepiga chenga nyingi mabeki wa kikosi cha kocha Malale Hamsini cha JKU.
Mara tu baada ya mechi hiyo, Goran aliiponda Simba iliyoanza na wachezaji wawili wa kigeni, Waganda Juuko Murushid na Dan Sserunkuma akidai bado ina tatizo la kukata pumzi.
Kocha huyo alisema: "Tunamshukuru Mungu kwa ushindi huu wa pili lakini timu yangu bado ina udhaifu mkubwa. Bado tuna tatizo la kukosa pumzi, wachezaji wanaonekana hawako fiti."
"Tumecheza vizuri hadi dakika ya 27 na baada ya hapo tukaonekana kuzidiwa na wapinzani wetu kutokana na pumzi yetu kuonekana ndogo. Ninajua chanzo cha tatizo hili, nitalitatua kwa mbinu ambazo siwezi kuziweka wazi kwa sasa," alisema zaidi Mserbia huyo.
Kundi C: P W L D GF GA GD PTS
1. Simba 3 2 1 0 2 1 1 6
2. Mtibwa 3 1 0 2 2 1 1 5
3. JKU 3 1 1 1 3 2 1 4
4. Mafunzo 3 0 2 1 O 3 -3 1