YAYA TOURE MCHEZAJI BORA AFRIKA

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya CAF ya mchezaji bora Afrika kwa mara ya nne mfululizo.


Toure, 31, alitajwa kuwania tuzo hiyo baada ya kutoa mchango mkubwa kwa Manchester City kushinda Ligi Kuu ya England na kunyakua Kombe la Ligi.
Pia aliisaidia Ivory Coast kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Toure alipambana na mshambuliaji kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama.
Toure pia alitajwa kuwania tuzo ya Ballon D'Or Oktoba mwaka 2014.

Mshambuliaji wa Everton Samuel Eto'o ni mchezaji mwingine pekee kuwahi kushinda tuzo ya CAF ya mchezaji bora Afrika mara nne, ingawa sio mfululizo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI