KAVUMBAGU AIHOFIA MTIBWA SUGAR

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Azam FC amesema timu za Yanga, Mtibwa Sugar na KCCA ya Uganda ndizo ziwapa wakati mgumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwaka huu.

Akizungumza na jijini hapa, Kavumbagu alisema timu hizo zinatisha.

"Yanga, KCCA na Mtibwa wako vizuri, si timu za kutamani ukutane nazo katika michuano hii. Yanga wameimarika, Mtibwa bado wako katika kiwango chao cha Ligi Kuu. Hii timu kutoka Uganda inacheza kwa ushirikiano sana," alisema Kavumbagu.

Mrundi huyo alitamba akiwa na Yanga, lakini aliruhusiwa kuondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake na akatua bure Azam.


Aliitungua goli moja timu yake hiyo ya zamani katika sare ya 2-2 ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara wiki mbili zilizopita.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA