Machapisho

Yanga Princess hoi kwa JKT Queens

Picha
Yanga Princess imeshindwa kutamba mbele ya JKT Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake mzunguko wa tatu uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, jijini Dar es Salaam. Yanga Princess iliyokuwa nyumbani imekubali kichapo cha bao 0-1 lililofungwa na Asha Mwalala kipindi cha kwanza. Matokeo hayo yanaifanya Yanga Princess kupoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kuanza vizuri kwa kuzifunga Bunda Girls na Geita Queens.

Ibenge achekelea Azam FC kutumia Amaan Stadium

Picha
Klabu ya Azam FC imepata chaguo la uwanja wa nyumbani kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa ya CAF Champions League. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, Azam FC inatarajiwa kutumia Uwanja wa Amani, Zanzibar, kama uwanja wake wa nyumbani katika michuano hiyo. Kocha mkuu wa Azam FC, Ibenge, anatarajiwa kutumia vizuri faida ya kucheza nyumbani katika michuano hiyo ya kimataifa. Uwanja wa Amani unaweza kuwa sehemu muhimu kwa Azam FC kuonyesha ubora wake, huku uzoefu wa kocha huyo ukiwa miongoni mwa mambo yanayoweza kuisaidia timu kufanya vizuri katika msimu wa 2026. Kwa upande mwingine, Azam FC pamoja na Young Africans (Yanga) watatumia Uwanja wa Amani, Zanzibar, kama uwanja wa nyumbani kwa ajili ya mechi zao za hatua ya makundi ya CAF Confederation Cup (CAF CC) na CAF Champions League (CAF CL), mtawalia. Wakati huohuo, Simba SC pamoja na Singida Black Stars (Singida BS) zitatumia Uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani. Hata hivyo, uwanja huo umewekewa sharti la k...

Sibusiso Makhula avaa viatu vya Musa Mgosi, Simba Queens

Picha
Kocha wa viungo kutoka timu kubwa ( Senior Team) Sibusiso Makhula amekiongoza kikosi katika mchezo wa leo dhidi ya Mashujaa Queens kutokana na Kocha Mkuu Mussa Hassan Mgosi kuwa katika kozi inayoendelea Jijini Tanga.

Rasmi, Yanga na Polisi Tz kucheza Ushirika Stadium

Picha
HATIMAYE fumbo la mahali utakapochezwa mchezo wa Polisi Tanzania dhidi ya Yanga, limepatiwa majibu baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kuthibitisha kuwa pambano hilo litapigwa kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, Novemba 20, 2026. Uthibitisho huo umekata mzizi wa tetesi zilizokuwa zikisambaa mitandaoni kuhusu uwezekano wa mchezo huo kuhamishiwa uwanja mwingine, huku mashabiki wa soka mkoani Kilimanjaro wakisubiri kwa hamu kuiona Yanga ikishuka dimbani kwenye ardhi yao. Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu, Kaimu Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi, Yahya Abushekhe, amesema hadi sasa hakuna mabadiliko yoyote kuhusu uwanja utakaotumika katika pambano hilo.

Awesu, Masawe warejea kuibeba Namungo FC

Picha
Kikosi cha Namungo FC kimepata habari njema baada ya viungo wake wazoefu, Jacob Masawe na Awesu Awesu, kurejea rasmi uwanjani na kuanza mazoezi mepesi. Nyota hao walikuwa nje ya dimba kwa muda mrefu wakiuguza majeraha ya misuli na goti yaliyowaweka kando katika michezo kadhaa iliyopita, ambapo klabu ya Namungo FC haikuweka wazi taarifa za kina za kitabibu hadi inapotangaza kurejea kwao. Kurejea kwa viungo hao kunaongeza nguvu kubwa katika benchi la ufundi la ‘Wauaji wa Kusini’ wakati wakijiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Novemba 20, 2026 kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.

CR7 kuongeza mkataba Al Nassr hadi 2029

Picha
Dunia ya soka inaweza kushuhudia historia nyingine kubwa. Ripoti zinaeleza kuwa nahodha wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, yupo tayari kusaini mkataba mpya utakaomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2029. Mpango huo unatajwa kuwa sehemu ya maandalizi ya kumwezesha Ronaldo kushiriki michuano ya FIFA Club World Cup, endapo Al-Nassr watafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Asia (AFC Champions League) msimu huu au msimu ujao. Inadaiwa kuwa viongozi wa Al-Nassr wameahidi kuimarisha kikosi kwa kusajili wachezaji wa kiwango cha juu duniani, ili kumpa Ronaldo timu yenye ushindani mkubwa na nafasi ya kuendelea kung'ara kwenye majukwaa makubwa ya soka duniani.

Infantinho aridhia wazo la Afrika

Picha
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amewaeleza viongozi wa shirikisho hilo kuwa ameamua kuondoa rasmi mpango wa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki Fainali za Kombe la Dunia 2030 kutoka timu 48 hadi timu 64. ​Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti maarufu la The Times nchini Uingereza, Infantino amewaarifu marais wa vyama vya soka vya mabara sita kuwa hatasukuma tena agenda hiyo ya ushirikiano wa timu 64 endapo atachaguliwa tena kuongoza FIFA katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 2027. Wazo hilo lililotolewa mwanzoni na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya Kombe la Dunia, limekutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mashirikisho makubwa kama UEFA na AFC. ​Desemba ya mwaka 2024, FIFA ilithibitisha kuwa fainali za 2030 zitafanyika kwa ushirikiano wa nchi za Morocco, Hispania, na Ureno, huku mechi tatu za ufunguzi zikipigwa nchini Uruguay, Argentina na Paraguay. Baada ya hatua hii ya Infant...