Yanga Princess hoi kwa JKT Queens
Yanga Princess imeshindwa kutamba mbele ya JKT Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake mzunguko wa tatu uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, jijini Dar es Salaam.
Yanga Princess iliyokuwa nyumbani imekubali kichapo cha bao 0-1 lililofungwa na Asha Mwalala kipindi cha kwanza.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga Princess kupoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kuanza vizuri kwa kuzifunga Bunda Girls na Geita Queens.
