Infantinho aridhia wazo la Afrika
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amewaeleza viongozi wa shirikisho hilo kuwa ameamua kuondoa rasmi mpango wa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki Fainali za Kombe la Dunia 2030 kutoka timu 48 hadi timu 64.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti maarufu la The Times nchini Uingereza, Infantino amewaarifu marais wa vyama vya soka vya mabara sita kuwa hatasukuma tena agenda hiyo ya ushirikiano wa timu 64 endapo atachaguliwa tena kuongoza FIFA katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 2027.
Wazo hilo lililotolewa mwanzoni na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya Kombe la Dunia, limekutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mashirikisho makubwa kama UEFA na AFC.
Desemba ya mwaka 2024, FIFA ilithibitisha kuwa fainali za 2030 zitafanyika kwa ushirikiano wa nchi za Morocco, Hispania, na Ureno, huku mechi tatu za ufunguzi zikipigwa nchini Uruguay, Argentina na Paraguay.
Baada ya hatua hii ya Infantino kusalimu amri, mfumo wa timu 48 uliotumiwa kwenye Kombe la Dunia 2026 utaendelea kutumika katika fainali hizo za kihistoria.
