CR7 kuongeza mkataba Al Nassr hadi 2029
Dunia ya soka inaweza kushuhudia historia nyingine kubwa. Ripoti zinaeleza kuwa nahodha wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, yupo tayari kusaini mkataba mpya utakaomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2029.
Mpango huo unatajwa kuwa sehemu ya maandalizi ya kumwezesha Ronaldo kushiriki michuano ya FIFA Club World Cup, endapo Al-Nassr watafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Asia (AFC Champions League) msimu huu au msimu ujao.
Inadaiwa kuwa viongozi wa Al-Nassr wameahidi kuimarisha kikosi kwa kusajili wachezaji wa kiwango cha juu duniani, ili kumpa Ronaldo timu yenye ushindani mkubwa na nafasi ya kuendelea kung'ara kwenye majukwaa makubwa ya soka duniani.
