Kangwanda abadili upepo Chipolopolo
KOCHA wa muda wa timu ya Taifa ya Zambia, George Lwandamina, amesema awali alikuwa na wasiwasi kuhusu Albert Kangwanda alipokwenda Yanga, lakini kiwango alichoonyesha tangu ajiunge na mabingwa hao wa Tanzania kimemfanya abadili mtazamo wake. Lwandamina, ambaye pia anafanya kazi na Kangwanda katika kikosi cha Chipolopolo, amesema historia ya wachezaji waliowahi kucheza Yanga ilimfanya kuwa na hofu kama kiungo huyo angeweza kukabiliana na presha ya klabu hiyo. Amesema pamoja na Kangwanda kuanza kuonyesha uwezo wake, bado anatakiwa kuongeza juhudi zaidi ili kuendelea kupata nafasi ya kuaminiwa na mashabiki wa Yanga. “Kwa kiwango chake cha sasa nimemwambia anatakiwa kuongeza juhudi zaidi, kwa sababu kama amekubalika na mashabiki wa Yanga basi ataweza kufanikiwa kirahisi zaidi,” amesema. Kangwanda alijiunga na Yanga Julai mwaka huu akitokea Red Arrows ya Zambia, ambako alikuwa ametoka kuwa na msimu bora wa 2025/26 akiwa na mabao 17 na asisti tisa katika mashindano yote. Lwandamina amesema a...