Ahmed Ally aisikitikia Yanga kukaa kimya dabi

“Inasikitisha sana inaumiza mno kuona wenzetu wapo kimya kama vile hakuna kinacho endelea siku ya hivi karibuni, wanacho kifanya watani wetu sio kitu Kizuri. Unajua Dabi ni mechi kubwa, mechi yenye hadhi ya juu. Dabi yetu ni kivutio Kizuri sana, ilibidi tuitunze kwa wivu mkubwa.

Miaka ya nyuma wiki ya Dabi huwa ya moto sana, tambo mbali mbali mtaani. Kila upande kujinasibu kushinda mchezo, lakini sasa hayo mambo hayapo tena. Yani watani zetu wamekaa kimya kama wanaenda kucheza na Timu ndogo ndogo hivi..

Wanacho fanya ni roho mbaya tu labda wanadhani wakiongea basi watatupa faida sisi watu kujaa uwanjani.. Hilo kwetu sio inshu, mashabiki watakuja kuunga mkono timu yao. Hata mashabiki wao wasipo kuja uwanjani, Uwanja utajazwa na Wana Simba pekee hakuna shida yoyote. Acheni waendelee kukaa kimya, zamu yao ikifika na sisi tutakaa kimya”

AHMED ALI.. Msemaji wa Simba Sc.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons