McCarthy aikatia tamaa Harambee Stars

Kocha Mkuu wa Harambee Stars ya Kenya, Benni McCarthy, amesema kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ni Jambo ambalo kwa sasa haiwezekani kwa Taifa hilo kutokana na ubora wa kikosi na rasilimali walizonazo.

McCarthy amesema hata kama angepewa mamilioni ya dola ili kuiwezesha Kenya kushinda AFCON, bado timu hiyo haina nguvu na rasilimali za kutosha kushindana kwa kiwango sawa na mataifa yenye nguvu barani Afrika kama Morocco, Misri, Senegal na Ivory Coast.

Kocha huyo amesema lengo la kwanza kwa Kenya katika AFCON 2027, ambayo itafanyika kwa pamoja Tanzania, Kenya na Uganda, linapaswa kuwa kuvuka hatua ya makundi na kufikia hatua ya robo fainali au nusu fainali, huku ushindani wa ubingwa ukiwa ni mpango wa muda mrefu.

McCarthy amesema Kenya inaweza kuhitaji hadi miaka 10 ya maendeleo kabla ya kuwa na uwezo wa kushindania ubingwa wa AFCON, akisisitiza kuwa kizazi kipya cha wachezaji wanaocheza nje ya nchi kinaweza kuwa msingi wa mafanikio hayo ya baadaye.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons