Simba na Yanga zapigwa stop Uhuru

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema Uwanja wa Uhuru hautatumika kwa mazoezi ya Simba wala Yanga kuelekea mchezo wa Dabi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 10, 2026.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 7, 2026, Wizara imesema hatua hiyo inalenga kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na Bodi ya Ligi kuhusu matumizi ya viwanja vya mashindano, hususan masuala yanayohusu mazoezi ya timu.

Wizara imesisitiza kuwa hakuna timu yoyote kati ya Simba na Yanga itakayoruhusiwa kutumia Uwanja wa Uhuru kwa mazoezi kabla ya mchezo huo, kwa kuzingatia matakwa ya kanuni za mashindano ya Ligi.

Aidha, Wizara imewataka wadau, Mashabiki wa Simba na Yanga pamoja na Watanzania kwa ujumla kuzingatia utulivu, amani na taratibu zilizowekwa kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons