Machapisho

Depu atambulishwa Petro de Luanda

Picha
Mshambuliaji raia wa Angola, Laurindo Aurélio maarufu Depu, ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Petro de Luanda baada ya kuondoka Yanga. Depu ametambulishwa rasmi leo Jumatano Agosti 12, 2026 ambapo inadaiwa Yanga imeingiza kitita cha dola 500,000 (Sh1.3 bilioni) kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyo. Depu alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu uliopita kabla ya kurejea nchini Angola kujiunga na Petro de Luanda.

Hadithi ya Seleman Mwalimu kuihama Simba usiku saa 9 na kwenda Yanga

Picha
-Kwamba Simba walikubaliana na Wydad Ac Usd 120,000 sawa na Milioni 316 kwajili ya mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja wa mchezaji Selemani Mwalimu. Simba walikuwa tayari kutoa hiyo pesa ndio maana mchezaji akaruhusiwa kurudi Tanzania na akafikia kwenye Kambi ya Simba ambako alikuwepo mpaka jana kwenye mazoezi ya Simba pale Zanzibar. Yanga walivyopata taarifa za Simba kuchelewa kufanya malipo, wakaulizia wakaweka mezani Usd 200,000 (Milioni 527) yaani Usd 80,000 zaidi ya ile pesa waliyokubaliana na Simba...Wydad wakampigia simu Mwalimu kumwambia awaambie Simba kuna timu imeweka 200,000 hivyo Simba waongeze Usd 30,000 tu iwe Usd 150,000 (Milioni 395) Selemani Mwalimu alivyowaambia viongozi wa Simba, wakamwambia wanawachekecha tu kwasababu Yanga hawana uhitaji wa mshambuliaji tena... Baadaye Viongozi wakampigia simu Mwalimu kumwambia wamemalizana na Yanga hivyo anatakiwa kurudi Dar, ndipo akaondoka na ndege ya usiku kurudi Dar na alisaini mkataba na Yanga saa 9:45 usiku. Usd 30,000 ndiyo il...

Simba timu ya kushinda mataji+ Barker

Picha
Nimependa namna kocha wa Simba Steve Barker anavyozungumza kwa kujiamini,anasema Simba ni timu ya kushinda mataji hivyo anaamini kesho watafanya hivyo pia dhidi ya Yanga. Maneno anayozungumza yana ukweli mkubwa ndani yake,hasa ukizingatia kile ambacho ameshakifanya na Simba msimu uliopita walishinda FA mbele ya Azam, timu ambayo ilitoka kuifunga Yanga,huu ni uthibitisho wa kwanza wa kocha anachokisema. Simba hawakushinda FA peke yake walishinda mechi ya fainali ya Kombe la Muungano ambalo walicheza na Yanga. Ukichukua matukio ya Simba msimu uliopita na kocha anachokisema ni wazi kuwa ana sababu za kuzungumza kwa kujiamini sio maneno matupu tayari kuna kitu alishakifanya yeye kama yeye,ukiachana na klabu.

Tizi la kwanza la Gomez Yanga

Picha
Tizi la kwanza la straika Seleman Mwalimu Gomez akiwa na kikosi cha Yanga... Hapa ni Zanzibar na haya ni maandalizi kuelekea game ya Ngao ya Jamii , Yanga vs Simba Agosti 12

Fofana kufunga usajili Yanga

Picha
Yanga wako kwenye mazungumzo na kiungo mshambuliaji wa Asec Mimosas,Souleymane Fofana (20). personal terms Siyo ishu na mchezaji yuko tayari kuja Yanga,ila Yanga watavunja mkataba wake baada ya mauzo ya Okello kukamilika. Yanga wana ofa ya $790,000 (Tsh 2b) kutoka nje ya nchi na punde pesa ikiwekwa kwenye akaunti OKello ataondoka na Yanga watakamilisha usajili wa Fofana.

Simba yajibu mapigo kwa Feitoto'

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wanakaribia kukamilisha moja ya sajili za kishindo zaidi nchini, Kiungo Mshambuliaji Feisal Salum. 🔥Rais wa Heshima wa Simba SC, Mohamed Dewji ‘MO’, kuweka TZS Bilioni 4 kwenye akanti ya klabu maalum kwa ajili ya kufanikisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’. Mbali na dau la kuvunja mkataba wake Azam FC linalotajwa kufikia TZS Bilioni 1 (Buy-out clause), Simba SC tayari wamefikia makubaliano binafsi (Personal Terms) na mchezaji huyo kupokea mshahara unaokadiriwa kuzidi TZS Milioni 70 kwa mwezi. Hatua hii kubwa kutoka kwa MO Dewji inakuja kama jibu la moja kwa moja kufuatia Simba SC kumkosa aliyekuwa mlengwa wao, Selemani Mwalimu, aliyejisajili na watani zao wa jadi, Yanga SC. 🧠 Taarifa za ndani zinaeleza kuwa changamoto kuu imekuwa kwenye mchakato wa majadiliano (negotiations) unaoendeshwa na safu ya uongozi, jambo lililokwamisha au kuchelewesha baadhi ya sajili kama ilivyotokea kwa Selemani Mwalimu, licha ya Boss huyo k...

Ahmed Arajiga akabidhiwa Ngao ya Jamii kesho

Picha
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua mwamuzi wa kimataifa wa FIFA, Ahmed Arajiga kutoka Manyara, kuwa Mwamuzi wa Kati (Center Referee) katika mchezo wa nusu fainali/fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Young Africans SC na Simba SC, utakaopigwa Jumatano, Agosti 12, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kuanzia saa 2:30 usiku. ​📋 Orodha Kamili ya Waamuzi wa Mchezo (Match Officials): ​REF (Mwamuzi wa Kati): Ah med Arajiga (Manyara) ​A1 (Mwamuzi Msaidizi wa Kwanza): Mohamed Mkono (Tanga) ​A2 (Mwamuzi Msaidizi wa Pili): Leonard Mkumbo (Manyara) ​RR (Mwamuzi wa Akiba / Reserve Ref): Nassir Siyah (Zanzibar) ​MC (Kamishna wa Mchezo / Match Commissioner): Hamis Kitila (Singida) ​RA (Tathmini ya Waamuzi / Referee Assessor): Soud Abdi (Arusha) ​Arajiga, ambaye ni mmoja wa waamuzi wenye uzoefu mkubwa katika mechi zenye shinikizo la juu nchini, anapewa dhamana nyingine kubwa ya kusimamia sheria 17 za soka katika Dabi hii ya Kariakoo inayotarijiwa kuwa ya vuta-ni...