Simba yajibu mapigo kwa Feitoto'


Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wanakaribia kukamilisha moja ya sajili za kishindo zaidi nchini, Kiungo Mshambuliaji Feisal Salum.

🔥Rais wa Heshima wa Simba SC, Mohamed Dewji ‘MO’, kuweka TZS Bilioni 4 kwenye akanti ya klabu maalum kwa ajili ya kufanikisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Mbali na dau la kuvunja mkataba wake Azam FC linalotajwa kufikia TZS Bilioni 1 (Buy-out clause), Simba SC tayari wamefikia makubaliano binafsi (Personal Terms) na mchezaji huyo kupokea mshahara unaokadiriwa kuzidi TZS Milioni 70 kwa mwezi.

Hatua hii kubwa kutoka kwa MO Dewji inakuja kama jibu la moja kwa moja kufuatia Simba SC kumkosa aliyekuwa mlengwa wao, Selemani Mwalimu, aliyejisajili na watani zao wa jadi, Yanga SC.

🧠 Taarifa za ndani zinaeleza kuwa changamoto kuu imekuwa kwenye mchakato wa majadiliano (negotiations) unaoendeshwa na safu ya uongozi, jambo lililokwamisha au kuchelewesha baadhi ya sajili kama ilivyotokea kwa Selemani Mwalimu, licha ya Boss huyo kutenga bajeti ya kutosha.

Uchanganuzi wa kina wa dili hili linaloenda kutikisa soka la Bongo: