Machapisho

Simba yaitumia salamu Esperance

Picha
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na winga mpya wa kushoto, Libasse Gueye (22) aliyesajiliwa mwezi huu katika dirisha dogo kutoka Teungueth FC ya kwao, Senegal dakika ya 27 na mshambuliaji Suleiman Abdallah Mwalimu 'Gomez' anayecheza kwa mkopo tangu mwanzo wa msimu kutoka Wydad Athletics dakika ya 76. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 16 katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya nne, wakati Mashujaa FC inabaki na pointi zake 13 za mechi 11 sasa nafasi ya nane. Baada ya mchezo huo, Simba SC inarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Espérance ya Tunisia Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Ili kufufua matumaini ya kwenda Robo Fainali, Simba inahitaji kushinda Jumapili ikitoka kufungwa mechi zote tatu ...

Uwanja wa KMC Complex wafungiwa

Picha
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu. Miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu. Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF. TFF inazikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja.

SIMBA INAAMINI LIGI YA MABINGWA AFRIKA INAANZA JUMAPILI!!

Picha
Na Prince Hoza Matua SIKU ya Jumapili ya tarehe 01, 02, 2026 wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, Simba SC watashuka uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuchuana na Esperance de Tunis ya Tunisia mchezo wa hatua ya makundi. Unatajwa kuwa ni mchezo wa muhimu sana kwa timu zote kwakuwa zinatafuta tiketi ya kucheza robo fainali, lakini ni muhimu zaidi kwa Esperance kwa sababu mpaka sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 5. Stade Malien ya Mali wanaongoza kwenye kundi lao lenye timu nne za Esperance ya Tunisia, Petro de Luanda ya Angola, Simba SC ya Tanzania na Malien, katika kundi hilo timu zote zimecheza mechi tatu na Malien ipo kileleni ikiwa na pointi 7. Esperance inayokutana na Simba Jumapili, inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 5, Petro de Luanda inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4 na timu inayoshika mkia ni Simba SC yenye pointi 0. Baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika ikiwa haina hata pointi moja, Si...

Mohamed Doumbia asajiliwa Marumo Gallants

Picha
Mohamed Doumbia ameondoka Yanga na kujiunga na Marumo Gallants,ya South Africa kwa mkopo. [1/28, 6:13 PM] Bro Big: Mohamed Doumbia, kiungo wa kati wa taifa la Ivory Coast, ameondoka Yanga SC ya Tanzania na kujiunga na klabu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa mkopo wa msimu mzima. Doumbia amekuwa na changamoto ya kupata dakika za kutosha kucheza Yanga kutokana na ushindani mkali katika safu ya kiungo. Mkopo huu unampa nafasi ya kupata dakika nyingi za kucheza na kuboresha kiwango chake.

Inno Jospin Loemba atambulishwa Simba

Picha
KLABU ya Simba SC imemtambulisha kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Kongo-Brazzaville, Iñno Jospin Loemba (21) kutoka Colombe Sport ya Cameroon. Simba SC imenasa saini ya mchezaji huyo ikizipiku klabu za Simba SC Wydad Casablanca ya Morocco, MC Algiers ya Algeria, Al Ahly FC na Pyramids FC zote za Misri. Loemba alijiunga na Colombe Sport Oktoba 2024 akitokea Inter Club, baada ya awali kuchezea AS Otôho kuanzia Agosti 2022 hadi Novemba 2023 akitokea JS de Talangai, zote za kwao, Kongo-Brazzaville. Loemba anakuwa anakuwa mchezaji mpya wa saba Simba SC dirisha hili dogo baada ya kipa Mahamadou Tanja Djibrilla Kassali Djibo (29) kutoka AS FAN Niamey ya kwao, Niger na beki wa kushoto mzawa, Nickson Clement Kibabage (25) kutoka Singida Black Stars ya nyumbani. Wengine ni beki wa kati, Ismaël Olivier Touré (28) kutoka FC Baniyas ya Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), winga wa kushoto Msenegal, Libasse Gueye (22) kutoka Teungueth FC ya kwao, winga wa kushoto, Muivory Coast, Anicet Our...

Sowah amuangukia Injinia Hersi

Picha
Mshambuliaji Jonathan Sowah amefunguka kwa majonzi, akieleza kosa analolijutia zaidi katika taaluma yake ya soka tukio linalosema bado linamwathiri kisaikolojia hadi leo. Sowah amesema aliwahi kuwa na ndoto ya kuichezea Yanga SC, ndoto iliyojengwa kupitia uhusiano wake wa karibu na Eng. Hersi Said, ambaye anamchukulia kama mzazi kutokana na mchango wake mkubwa tangu akiwa Medeama. Ndoto hiyo ilizidi kuimarika baada ya kuvutiwa na mapokezi ya mashabiki wa Yanga alipofika Dar es Salaam. Hata hivyo, baada ya kukosa mwendelezo wa mawasiliano, alikubali kujiunga na Singida Black Stars kwa ushauri wa Hersi, akiamini ingetumika kama daraja. Mambo yalibadilika baada ya kupata ofa ya Simba SC, aliyoichagua kwa sababu za kujitangaza kimataifa. Tukio analolijutia zaidi ni kuchana picha ya Rais wa Yanga wakati wa utambulisho wake Simba akitaja kuwa hakufanya kwa hiari bali kwa shinikizo la mazingira. Kwa unyenyekevu, Sowah ameomba radhi kwa Eng. Hersi Said, akisisitiza bado anamheshimu kama mzazi ...

Singida Black Stars waifuata AS Otoho Brazzavile

Picha
Kikosi cha Singida  Black Stars kutoka mkoani Singida kinatarajiwa kutua jijini Brazzaville nchini Congo Brazzaville, mapema kwa ajili ya kuanza maandalizi yao ya mwisho mwisho kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya AS Otoho. Singida Black Stars wameondoka nchini Alfajiri ya leo kuelekea kwenye mchezo huo kupitia Katika njia ya jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. AS Otoho na Singida Black Stars zitashuka dimbani Februari 1 mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni. Kama Singida Black Stars watapata ushindi wowote kwenye mchezo huo watafikisha alama saba na itakuwa wamewasha alama ya kijani kuelekea kufuzu hatua ya Robo Fainali. Singida Black Stars imeondoka na wachezaji wake 21 kwa ajili ya mchezo huo huku ikiwa na wachezaji sita ambao wameingia kwenye kikosi hiko katika dirisha dogo la usajili huku Khalid Aucho bado anatazamwa kama mchezaji mzoefu kwenye kikosi hiko