Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni kama
ilivyoainishwa kwenye masharti ya
Kanuni ya Leseni za Klabu.
Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika
kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa
baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.
TFF inazikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja.
