Kikosi cha Singida Black Stars kutoka mkoani Singida kinatarajiwa kutua jijini Brazzaville nchini Congo Brazzaville, mapema kwa ajili ya kuanza maandalizi yao ya mwisho mwisho kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya AS Otoho.
Singida Black Stars wameondoka nchini Alfajiri ya leo kuelekea kwenye mchezo huo kupitia Katika njia ya jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.
AS Otoho na Singida Black Stars zitashuka dimbani Februari 1 mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni.
Kama Singida Black Stars watapata ushindi wowote kwenye mchezo huo watafikisha alama saba na itakuwa wamewasha alama ya kijani kuelekea kufuzu hatua ya Robo Fainali.
Singida Black Stars imeondoka na wachezaji wake 21 kwa ajili ya mchezo huo huku ikiwa na wachezaji sita ambao wameingia kwenye kikosi hiko katika dirisha dogo la usajili huku Khalid Aucho bado anatazamwa kama mchezaji mzoefu kwenye kikosi hiko



