Yanga na Wydad Casablanca kuchuana Wiki ya Wananchi, Diamond ndani.....
Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC itacheza na timu ya Wydad Casablanca ya Morocco katika siku ya kuadhimisha tamasha lake la Wiki ya Wananchi Agosti 4 mwaka huu. Yanga SC itaadhimisha tamasha lake la Wiki ya Wananchi katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo pia msanii nambari moja Afrika mashariki Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz atapanda jukwaani. Wydad Casablanca ni moja kati pendwa barani Afrika hivyo kualikwa na Yanga kutalifanya tamasha hilo kufana kwani tayari Yanga imeshatoa viliingilio vya kuuona mchezo huo ambao utakuwa mahsusi kwa kutambulisha usajili wao msimu ujao