Mke wa Mwaitege akanusha kifo cha mumewe
Mke wa Mwimbaji wa nyimbo za injili Nchini Tanzania Boniface Mwaitege amekanusha taarifa zilizosambazwa mitandaoni na kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari kuwa Mumewe Boniface amefariki leo.
Akiongea leo July 22,2024 Mke wa Mwaitege amenukuliwa akisema yafuatayo ———> “Bony Mwaitege ni mzima kabisa ametoka safari kutoka Kenya na amefika nyumbani salama, amepumzika”
Baadhi ya Mitandao leo iliripoti kuwa Mwimbaji huyo amefariki kutokana na ajali ya barabarani kitu ambacho Mkewe amesema kuwa ni uongo na uzushi.
