Kibu aibukia Norway
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC Kibu Denis "Kibu" anarajia kujiunga na klabu moja ya Ligi Kuu nchini Norway ambapo kwasasa yupo huko na mipango ikikamilika dili lake litakuwa limeisha.
Inasemekana wakala wake atawasiliana na klabu yake ya sasa ya Simba na watakubaliana ili kuvunja mkataba ama klabu inayomtaka iweze kumalizana na Simba.
Dili la Kibu na klabu mpya atakayojiunga nayo ni kubwa kuliko ile ya klabu yake ya sasa, na ndio maana ajajiunga na wenzake huko Ismailia Misri
