MAKALA: Mashabiki wa soka nchini wajifunze kushangilia
Na Prince Hoza SIKU kumekuwa na tabia mbaya hasa kutoka kwa mashabiki wa soka hapa nchini kujifanya wakosoaji badala ya kusimama kwenye maeneo yao ya ushangiliaji. Mashabiki wa soka hasa wa hapa nchini, wamekuwa wakisifika kwa kupenda sana mchezo huo na kuisaidia nchi kuonekana ina mashabiki wengi wanaoufuatilia zaidi mchezo huo. Lakini bahati mbaya, mashabiki wa soka wa hapa nchini wanaishia kujitokeza kwa wingi viwanjani na hata kwenye vibanda umiza, yote kuzisapoti timu zetu lakini hawajui kushangilia kama inavyotakiwa na zaidi wamejikita kwenye kukosoa. Yaani mashabiki wa soka nchini wamegeuka wachambuzi na badala yake wamekuwa wakikosoa timu zao, wapo mashabiki wamejifanya wakosoaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, hasa wakimkosoa kocha mkuu wa timu hiyo katika uteuzi wake alioufanya hivi karibuni. Pia wapo wengine wakimkosoa kocha wa timu ya Simba SC, Robert Olveira "Robertinho", na wengine wanamkosoa kocha wa timu ya Yanga SC Nasreddine Nabi, kwa kifupi mashabiki wa...