Stars kamili kuiua Uganda kesho
Na Ikram Khamees
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania leo hii kimeendelea na mazoezi tayari kwa kujiandaa kuelekea mchezo wa marudiano wa kufuzu AFCON dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda, mchezo huo utachezwa siku ya Jumanne ya tarehe 28/03/2023 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Tanzania.
Kwahiyo kocha Adel alikuwepo miezi miwili kabla ya
kutangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania kama anavyosema Rais wa shirikisho la mpira wetu TFF Wallace Karia? na alikuwa anawatazama baadhi ya wachezaji wakati ligi zinaendelea, sasa ndani ya hiyo miezi miwili hakuona umuhimu na ubora wa walinzi wawili wa pembeni Shomari Kapombe na Mohamed Hussein?.
Badala yake akaona ubora wa kina Datus Peter, Kibwana Shomari kama mabeki wa kulia, na kushoto akawaona David Charles Luhende na Yahya Suleiman Mbegu? kwahiyo kocha aliangalia zaidi mechi za Kagera Sugar na Ihefu kuliko mechi za Simba? maana kwa maelezo ya Rais wetu wa heshima kasema hata kikosi ni mwalimu alikiita.
Na ukiangalia wachezaji walioitwa awali kwenye nafasi ya Shomari Kapombe na Mohamed Hussein kwa maana ya mbavu ya kulia Kibwana Shomari na Datus Peter, na mbavu ya kushoto Yahya Mbegu na David Luhende, hakuna hata mchezaji mmoja ambaye alianza au kupata nafasi kwenye mchezo uliopita, badala yake wakacheza wachezaji ambao mara nyingi wamekuwa wakicheza kwenye maeneo mengine tofauti na kucheza kama walinzi wa pembeni, kwahiyo waliitwa lakini bado mwalimu hajawa na imani ya kuwapa mechi kubwa na yenye umuhimu, je bado tunajaribu kikosi wakati tupo kwenye wakati wa kutafuta matokeo ili tufuzu, kweli tumejiandaa?
Sina shaka na uwezo wa hao walinzi walioitwa awali kabla ya Shomari Kapombe na Mo Hussein kuongezewa, wana ubora wao kama wachezaji wa madaraja ya kati lakini bado wana mengi ya kujifunza kwa hawa walinzi wawili wa Simba karibu katika kila maeno, speed, skills, uwezo wa kupiga pass, jumlisha majitoleo hasa kwenye mechi ngumu, Taifa letu bado halina wachezaji wengi wenye muendelezo wa ubora inabidi tuzoee tu kuona wachezaji karibu miaka yote hao hao, na kuna muda hawawi hao hao tu, ni hao hao na unakuta bado wana kitu mguuni.



