MAKALA: Mashabiki wa soka nchini wajifunze kushangilia

Na Prince Hoza

SIKU kumekuwa na tabia mbaya hasa kutoka kwa mashabiki wa soka hapa nchini kujifanya wakosoaji badala ya kusimama kwenye maeneo yao ya ushangiliaji. 

Mashabiki wa soka hasa wa hapa nchini, wamekuwa wakisifika kwa kupenda sana mchezo huo na kuisaidia nchi kuonekana ina mashabiki wengi wanaoufuatilia zaidi mchezo huo. 

Lakini bahati mbaya, mashabiki wa soka wa hapa nchini wanaishia kujitokeza kwa wingi viwanjani na hata kwenye vibanda umiza, yote kuzisapoti timu zetu lakini hawajui kushangilia kama inavyotakiwa na zaidi wamejikita kwenye kukosoa. 



Yaani mashabiki wa soka nchini wamegeuka wachambuzi na badala yake wamekuwa wakikosoa timu zao, wapo mashabiki wamejifanya wakosoaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, hasa wakimkosoa kocha mkuu wa timu hiyo katika uteuzi wake alioufanya hivi karibuni. 

Pia wapo wengine wakimkosoa kocha wa timu ya Simba SC, Robert Olveira "Robertinho", na wengine wanamkosoa kocha wa timu ya Yanga SC Nasreddine Nabi, kwa kifupi mashabiki wamekuwa wakosoaji kwa kila namna. 

Wakati wao wakijifanya wakosoaji ikiwa nao wana jukumu kubwa kuhakikisha timu zao zinafanya vizuri ikiwemo kushinda mataji, mashabiki nao wanahesabika kama wachezaji wa 12 na wanashiriki sawa kusababisha timu inapata matokeo. 

Tumejifunza kwa mashabiki wa nchi za Afrika kaskazini, ambao timu zao zimetuacha mbali sana, mashabiki wa huko wakiingia uwanjani kusapoti timu zao, bila kujali timu zao zimefungana au laah!, lakini wanashangilia kuanzia kipindi cha mwanzo hadi mwisho. 

Mashabiki wa wenzetu hawaangalii mpaka lipatikane goli ndio waanze kushangilia kama wanavyofanya mashabiki wetu, mashabiki wanajua kabisa wao wanabeba jukumu zito la kuwapa hamasa wachezaji. 

Inanishangaza sana mashabiki wetu wakienda uwanjani aidha wa timu ya Simba wanamsubiri Clatous Chama au Saido Ntibanzokiza wafanye mambo yao ndiyo waanze kushangilia, mbaya zaidi mashabiki wetu hugeuka mabubu kama timu yao haijapata goli na muda wote huwa kimya. 

Mashabiki wetu wanasubiri goli na chenga nyingi na pasi hapo utawaona wakishangilia kwa nguvu, lakini wanachofanya siyo sawa na wanatakiwa kujifunza kwa wenzetu waliopiga hatua. 



Hata kwa upande wa mashabiki wa Yanga nao wanasubiri liingie goli waanze kushangilia, mashabiki wa Yanga utawakuta jukwaani wamekaa kimya,  mashabiki hao wanamsubiri Fiston Mayele afunge ili wamuone anavyotetema. 

Wananisikitisha sana, hawajui kuwapa hamasa wachezaji wao, wenzetu waliopiga hatua, wakiingia uwanjani moja kwa moja wanaanza kushangilia timu yao ili kuwatia hamasa wachezaji hao. 

Hata kama timu yao imefungwa goli la kwanza au la pili, wao kazi yao ni kushangilia ili kuwatia hamasa waweze kusawazisha mabao, timu hata kama imefungwa wao wanaendelea kuwapa hamasa wachezaji wao.

Lakini mashabiki wetu timu ikifungwa wanakaa kimya na baadaye kukosoa wakati kazi ya kukosoa wenyewe wachambuzi. 

ALAMSIKI

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI