Machapisho

Gor Mahia kuleta yosso kombe la Kagame

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Uongozi wa mabingwa wa Sportpesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya umesema utaleta wachezaji vijana yaani yosso katika mashindano ya mwaka huu ya kombe la Kagame kwa kuhofia nyota wake kuumia kwani wanajiandaa na kombe la Shirikisho. Kauli hiyo imetokana na mapendekezo ya kocha mkuu Mwingereza Dylan Kerr ambapo amedai kikosi chake kinajiandaa na mchezo wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Yanga Sc ya Tanzania Julai 18 mwaka huu hivyo hawataleta kikosi chao cha kwanza. Pia wataenda Uingereza kucheza na Everton mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliotokana na kutwaa ubingwa wa shindano la Sportpesa, tayari timu za Yanga Sc na Saint George ya Ethiopia zimejitoa kushiriki kombe la Kagame na Gor Mahia inatoa kauli hiyo hivyo inaonyesha michuano hiyo itakosa msisimko

Ubelgiji yaishushia mvua ya magoli Panama, Sweden nayo yajipigia Korea Kusini

Picha
Timu ya taifa ya Ubelgiji imefanikiwa kuilaza Panama mabao 3-0 mchezo wa kundi G kombe la dunia nchini Urusi na kukamata usukani wa kundi hilo lenye timu za Tunisia na Uingereza ambazo zinaumana muda mfupi ujao. Magoli mawili ya nyota wa Manchester United Romelu Lukaku na moja la Dries Mertens yametosha kabisa kuipa pointi tatu muhimu timu hiyo yenye kiu na kombe hilo, mchezo uliopigwa saa tisa alasiri ulishuhudia Sweden ikianza vema fainali hizo baada ya kuilaza Korea Kusini bao  1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na nahodha wake Andreas Granqvist. Mchezo mwingine unatarajia kupigwa usiku huu kuanzia saa 3 kati ya Uingereza na wawakilishi wa Afrika Tunisia mchezo ambao unatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na umuhimu wa timu zote mbili

Kispoti

Picha
Preck "Mpole" ni mwanamuziki amenitoa machozi KWA mshangao mkubwa leo nimetoka nje ya mada, hapa huwa nazungumzia michezo, sijawahi kutoka nje ya mada tangu nilipoanza kuandika, lakini leo mtanisamehe wapenzi wasomaji kwa kushindwa kusimulia ya michezo. Sijatoka sana kwenye michezo kwani nilichoandika kinashabihiana na michezo, leo nimeandika makala inayohusu muziki na michezo ni sawa na uji na mgonjwa, kwa maana hiyo sijatoka sana nje ya mada. Lakini nimeamua kuiandikia makala hii baada ya kuguswa na simulizi ya msanii Mkwanda Mbwana Hamisi ambaye anajiita Preck Mpole kama jina lake la kisanii, bado hajawa supastaa kama akina Diamond Platinum, Ali Kiba, Mr Blue,  Chid Benz au T.I.D, ni msanii anayekuja ama anayechipukia. Katika mazungumzo yake na mimi, msanii huyo alizungumza mambo mengi lakini alinigusa pale alipoweza kusimulia kifo cha baba yake mzazi, Preck Mpole anasema mtu pekee aliyekuwa akimtegemea katika masomo ni baba yake mzazi,  kwani alibahatika kufaulu elimu...

NI VITA YA WAAFRIKA WENGINE NA WAUZA SURA ENGLAND

Picha
Mtifuano wa fainali za kombe la dunia bado inapamba moto huko Urusi na leo zinapigwa mechi tatu za kusisimua lakini ya kwanza ilikuwa kati ya Sweden na Korea Kusini katika uwanja wa Nizhni Novgorod Arena. Mechi itakayokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wengi ni kati ya wawakilishi wa Afrika Tunisia na wauza sura England, England inapigiwa chapuo kubwa na vyombo vya habari duniani hivyo inasubiriwa sana kwa hamu, mchezo huo utapigwa uwanja wa Volgograd Arena, lakini mechi hiyo ni ya usiku kuanzia saa 3:00. Mechi nyingine itapigwa jioni ya leo ni kati ya Ubelgiji na Panama nchi ambayo imefuzu kwa mara ya kwanza kushiriki fainali hizo na wananchi wake wote leo watakaa katika luninga kutazama timu yao nini inafanya, mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Sochi Stadium

Brazil yabanwa mbavu na Uswisi

Picha
Timu ya taifa ya Brazil usiku huu imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na watunza fedha wa Uswisi mchezo wa kundi E kombe la dunia uliofanyika katika uwanja wa Rostov On Don Arena. Ikicheza mbele ya mastaa wake Neymar Dos Santos anayekipiga Paris Saint Germany ya Ufaransa na Gabriel Jesus wa Man City ya England ilianza kujipatia bao la kuongoza kunako dakika ya 20 kipindi cha kwanza lililofungwa na kiungo Philipo Coutinho anayeichezea FC Barcelona ya Hispania. Lakini goli hilo lilidumu hadi kipindi cha pili kunako dakika ya 50 pale Steven  Zuber alipoisawazishia Uswisi na kufanya matokeo kuwa 1-1 huku kila timu ikiambulia pointi moja. Michuano hiyo itaendelea tena kesho ambapo majira ya saa 9 alasili, Sweden itaumana na Korea Kusini na jioni saa 12 Ubelgiji itachuana na Panama  wakati usiku saa 3, England itaumana na Tunisia ambao ni wawakilishi wa Afrika

Ujerumani yalala kwa Mexico, Serbia mwendo mdundo

Picha
Fainali za kombe la dunia zinazidi kunoga huko Urusi baada ya jioni ya leo mabingwa watetezi Ujerumani kuchapwa bao 1-0 kutoka kwa Mexico, mchezo wa kundi F uliopigwa uwanja wa Luzjhinski jijini Moscow. Mtu aliyepeleka huzuni Ujerumani leo alikuwa si mwingine ni Hirving Lazano kunako dakika ya 35 na kuondoka na pointi zote tatu, mchezo wa kwanza uliopigwa mchana wa leo ulizikutanisha Costa Rica na Serbia zikizo kundi E. Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Samara Arena, Serbia ilichomoza na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na A Kolarow kunako dakika ya 56, mechi nyingine inaendelea sasa kati ya Brazil na Uswisi kundi F kwenye uwanja wa Roston On Don Stadium

SINGIDA UNITED YAENDELEA KUIBOMOA TANZANIA PRISONS, YAMNASA KIUNGO NYOTA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Matajiri wa kulima Alizeti, timu ya Singida United leo tena imemtambulisha kiungo mshambuliaji Eliuta Herman Mpepo na kumtangaza rasmi kuwa mchezaji wake baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili. Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga  amemtambulisha mchezaji huyo ambaye alikuwa moto wa kuotea mbali katika kikosi cha Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya, lakini anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa akitokea kwa maafande hao wa jeshi la Magereza. Mara ya kwanza Singida United ilimtambulisha kiungo Kazungu Mashauri ambaye naye alisaini miaka miwili, Sanga amesema usajili wa Mpepo ni sehemu ya kukiimarisha kikosi chao ambacho msimu ujao kitakuwa chini ya Hemed Morocco aliyechukua mikoba ya Mholanzi Hans Van der Pluijm aliyehamia Azam Fc. Tayari wana fainali hao wa kombe la TFF maarufu Azam Sports Federation wameshakamilisha usajili wa nyota wengine sita ambao ni Danny Lyanga, Tibar John, Felipe Dos Santos, Amarra Diaby, Habibu Kiyombo na Mashauri ...