Ubelgiji yaishushia mvua ya magoli Panama, Sweden nayo yajipigia Korea Kusini

Timu ya taifa ya Ubelgiji imefanikiwa kuilaza Panama mabao 3-0 mchezo wa kundi G kombe la dunia nchini Urusi na kukamata usukani wa kundi hilo lenye timu za Tunisia na Uingereza ambazo zinaumana muda mfupi ujao.

Magoli mawili ya nyota wa Manchester United Romelu Lukaku na moja la Dries Mertens yametosha kabisa kuipa pointi tatu muhimu timu hiyo yenye kiu na kombe hilo, mchezo uliopigwa saa tisa alasiri ulishuhudia Sweden ikianza vema fainali hizo baada ya kuilaza Korea Kusini bao  1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na nahodha wake Andreas Granqvist.

Mchezo mwingine unatarajia kupigwa usiku huu kuanzia saa 3 kati ya Uingereza na wawakilishi wa Afrika Tunisia mchezo ambao unatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na umuhimu wa timu zote mbili

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons