Brazil yabanwa mbavu na Uswisi

Timu ya taifa ya Brazil usiku huu imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na watunza fedha wa Uswisi mchezo wa kundi E kombe la dunia uliofanyika katika uwanja wa Rostov On Don Arena.

Ikicheza mbele ya mastaa wake Neymar Dos Santos anayekipiga Paris Saint Germany ya Ufaransa na Gabriel Jesus wa Man City ya England ilianza kujipatia bao la kuongoza kunako dakika ya 20 kipindi cha kwanza lililofungwa na kiungo Philipo Coutinho anayeichezea FC Barcelona ya Hispania.

Lakini goli hilo lilidumu hadi kipindi cha pili kunako dakika ya 50 pale Steven  Zuber alipoisawazishia Uswisi na kufanya matokeo kuwa 1-1 huku kila timu ikiambulia pointi moja.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho ambapo majira ya saa 9 alasili, Sweden itaumana na Korea Kusini na jioni saa 12 Ubelgiji itachuana na Panama  wakati usiku saa 3, England itaumana na Tunisia ambao ni wawakilishi wa Afrika

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons