Simba kazini tena na Mwadui leo
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Simba SC inatarajia kushuka dimbani jioni ya leo kucheza na Mwadui FC kutoka Shinyanga katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na timu zote kuhitaji pointi tatu muhimu, Simba wao wana pointi nne na wanahitaji ushindi ili kuisogelea Mtibwa Sugar inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi tisa. Mwadui nao ambao wana pointi tatu wanahitaji ushindi ili kufikisha pointi sita, Simba inaingia uwanjani ikiwa na pengo la kiungo wake wa kimataifa, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ambaye ameumia, lakini Mganda Emmanuel Okwi ataongoza mashambulizi. Mbeya City nayo itacheza na Njombe Mji katika muendelezo huo wa Ligi Kuu Bara, mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Wachezaji wa Simba leo jioni wanacheza na Mwadui