Yanga vitani kesho bila Kamusoko

Na Exipeditor Mataruma. Songea

Klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga SC kesho Jumamosi itashuka uwanjani kucheza na Majimaji ya Songea katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mabingwa hao wanashuka uwanjani wakiwa na pengo la kiungo wao Mzimbabwe Thabani Scara Kamusoko ambaye ametonesha nyonga mazoezini jana na kushindwa kuendelea na mazoezi.

Kamusoko aliumia nyonga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji uliofanyika Jumapili iliyopita katika uwanja wa Sabasaba na Yanga kushinda bao 1-0 goli lililofungwa na Ibrahim Ajibu

Thabani Kamusoko huenda akaukosa mchezo wa kesho

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons