MTIBWA SUGAR YAZIDI KUPAA KILELENI,YAIZABA MBAO 1-0

Na Ikram Khamees. Morogoro

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea leo kwa kupigwa mechi tano ambapo Mtibwa Sugar imezidi kupaa kileleni baada ya kuichakaza Mbao FC ya Mwanza bao 1-0 katika Uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro.

Goli pwkee la Mtibwa Sugar lilifungwa na Kevin Sabato "Kiduku", kwa matokeo hayo Mtibwa imefikisha pointi tisa ikikamata uongozi na hakuna timu itakayoweza kuipoka nafasi hiyo kwa juma hili hata kama Simba kesho ikiifunga Mwadui.

Matokeo yote kwa ujumla haya hapa.

Majimaji 1 Yanga 1. (Majimaji Stadium), Lipuli 0 Ruvu 0, (Samora Stadium),  Prisons 0 Ndanda 0. (Sokoine Stadium), Mtibwa 2, Mbao FC, 1. (Manungu Complex) na Stand 0,  Singida United 1, (Kambarage).

Mtibwa Sugar inaongoza Ligi Kuu Bara

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons