Mtibwa na Yanga hakuna kulala
Na Ikram Khamees. Morogoro Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo inaendelea tena kwa Mtibwa Sugar kuikaribisha Yanga SC katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro mishale ya saa 10:00. Mchezo huo umekuwa gumzo kutokana na historia ya vilabu hivyo viwili kutambiana kila zinapokutana, Yanga ina rekodi nzuri ya kuifunga Mtibwa hasa ikicheza Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mtibwa nao wamekuwa na rekodi nzuri wanapokutana na Yanga katika uwanja wa Jamhuri, lakini msimu uliopita Yanga iljvunja mwiko kwa kuilaza Mtibwa mabao 2-0 kwenye uwanja huo huo wa Jamhuri. Kikosi cha Yanga kitaingia na taadhali hasa wakiangalia ushindani uliopo sasa, Yanga ikishinda mchezo huo itakaa kileleni na kuiangusha Simba inayoongoza kwa pointi 55, Yanga inajivunia straika wake Obrey Chirwa ambaye anacheza leo kufuatia kufutwa kwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa na mwamuzi Ahmad Simba dhidi ya Ruvu Shooting Jumatano iliyopita