Wezi wavunja nyumba ya John Terry na kuiba

Wezi wanaaminika kuvunja na kuingia katika nyumba ya aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza John Terry wakati akiwa katika likizo ya kifamilia.

Maafisa wa polisi wa Surrey walithibirisha kwamba nyumba iliyopo Oxshott ilivunjwa wikiendi iliyopita, John Terry ameripotiwa kuishi katika nyumba ya vyumba saba nchini humo.

Msemaji wa kituo hicho cha polisi wa Surrey amesema kuwa "Tunaweza kuthibitisha kuwa wizi ulifanyika katika nyumba moja iliyopo Moles Hill, Oxshott usiku wa tarehe 25 na 26 mwezi Februali mwaka huu", alisema msemaji wa polisi.

Wezi hao wanadaiwa kuvunja na kuingia katika nyumba hiyo na kuiba viru vyenye thamani wakati ambapo mchezaji huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 36 alikuwa ameenda likizo na watu wa familia akiwemo mkewe Toni kulingana na ripoti za gazeti la The Sun

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons