KESSY AMWITA MANARA IBILISI

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Beki wa pembeni wa Yanga, Hassan Ramadhan Kessy amesema hataki kujibizana na Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara na badala yake anamjibu kwa vitendo ndani ya uwanja kama alivyofanya Jumatano iliyopita alipocheza vizuri dhidi ya Ruvu Shooting na kuiongoza Yanga kushinda 2-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kessy aliitoa kauli hiyo mara baada ya mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, beki huyo alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Mzambia George Lwandamina. Beki huyo tangu atue Yanga hakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na mara kadhaa amekuwa akitokea benchi katika timu hiyo.

Kessy amesema aliiona na kuisoma post ya Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilikuwa ikimdhihaki kutokana na kukas benchi.

Kessy alisema baada ya kuisoma hakutaka kumjibu na badala yake slikaa kimya kuhofia majibizano yasiyokuwa na maana na badala yake akili zake alizielekeza kwenye kucheza soka pekee.

"Hivi vitu vinavyotokea hivi sasa kutoka kwa viongozi wa Simba akiwemo huyo Manara nilivitarajia tangu natoka Simba ninakuja kuichezea Yanga", amesema Kessy.

"Nakumbuka mwanzoni wakati nasaini kuichezea Yanga nilikuwa najibizana nao kwenye vyombo vya habari, lakini baada ya kugundua kuwa ninatoka mchezoni ninapojibizana nao, nikaamua kukaa kimya", aliongeza.

"Hivyo, sitaki kumkaribisha ibilisi hivi sasa na badala yake nitakaa kimya nikifanya kazi yangu ndani ya uwanja kwa kuwajibu kuonyesha kiwango kikubwa kwa lengo la kuipa ubingwa timu yangu ya Yanga", alisema Kessy

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons