Machapisho

DRC yailipua Morocco, Afcon

Picha
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeweka matatizo yake pembeni na kuicharaza Morocco kwa bao 1-0 kwenye mchezo wake wa ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon. Kikosi cha Froribert Ibenge kilchofanya mgomo siku ya Ijumaa kutokana na kutolipwa bakshishi zao, almanusura wafungwe bao la mapema kwenye Uwanja wa Stade d'0yere, baada ya Mbarak Boussoufa kugongesha mwamba shuti lake. Junior Kabanaaga ndiye aliyewainua mashabiki wa DRC baada ya kufunga bao pekee katika dakika ya 55 kipindi cha pili, DRC walimaliza wakiwa mchezaji mmoja pungufu baada ya Lomalisa Mutambala kutolewa nje kwa kuonyeshwa kadi mbili za manjano. Mutambala aliingia kama mchezaji wa akiba, na kutolewa baada ya dakika 16, Youssef El Araba wa Morocco alishindwa kufunga katika nafasi mbili alizopata kwa kichwa, mwishoni mwa mchezo. DRC walilazimika kucheza wakiwa tisa tu uwanjani kwa muda baada ya Mutambala kutolewa na beki Gabriel Zakuani kuumia na kutoka nje, Congo Kinshasa sasa inaongoza kundin...

Senegar yaanza kwa kutoa kichapo Afcon, leo ni Ivory Coast na Togo ya Bossou

Picha
Senegar wameanza vema michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tunisia katika kundi B. Tunisia wangeweza kupata bao katika dakika ya pili ya mchezo, pale Ahmed Akaichi alipipata fursa nzudi na kuupiga mpira kupitia kichwa lakini akatoka nje. Senegar ilipata bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na winga Sadio Mane. Tunisia walikosa nafasi nyingi za wazi hasa Youssef Msakni, ushindi wa vijana wa Allou Cisse umeifanya timu hiyo kuwa kileleni mwa msimamo  wa kundi lao. Zimbabwe nao walitoka sare ya 2-2 na Algeria kwa magoli ya Kudakwashe Mahachi na Nyasha Mushekwi na yale ya Riyad Mahrez yalitosha kukifanya pambano hilo kuwa droo, Leo Togo na Ivory Coast zimeumana vikali na hadi mwisho zilitoka suluhu 0-0

Ngoma aanzisha mgomo baridi Yanga

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Imebainika mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zimbabwe, Donald Ndombo Ngoma ameanzisha mgomo binafsi wa kukataa kucheza mechi yoyote akisingizia majeraha ya kifundo cha mguu. Ngoma anayekipiga Yanga SC akiwa amepachika jumla ya mabao manane, ameanza kugoma kuichezea timu hiyo tokea mchezo wao na Jamhuri ya Pemba katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyokuwa ikifanyika visiwani Zanzibar. Inadaiwa mshambuliaji haelewani vizuri na kocha wa kikosi hicho cha Wanajangwani Mzambia George Lwandamina, Ngoma akakosa mechi tatu dhidi ya Zimamoto Yanga ikishinda 2-0, dhidi ya Azam Yanga ikifungwa 4-0 na dhidi ya Simba iliyomalizika kwa sare 0-0 kisha Yanga kulala kwa matuta 4-2. Pia mshambuliaji huyo ameshindwa kuambatana na wenzake walioifuata Majimaji ya Songea mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kesho Uwanja wa Majimaji mjini Songea, taarifa zenye uhakika zinadai Ngoma anamgomo baridi dhidi ya Lwandamina na sababu haijajulikana ingawa Mambo Uwanjani inajua N...

Blagnon atimkia Fanja ya Oman

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba SC Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast, ametimkia Uarabuni kujiunga na timu ya Fanja FC ya Oman. Taarifa za kuondoka Blagnon zilienea leo ambapo baadaye msemaji wa Simba Haji Manara akathibitisha kuondoka kwa straika huyo aliyesajiliwa kwa mbwembwe. Blagnon analipwa na Simba shilingi milioni 6 na ndiye mchezaji ghari kwenye Klabu hiyo, lakini anajiunga kwa mkopo Fanja FC ambayo juzi imewasajili Mbuyu Twite na Kipre Balou. Simba imemruhusu Blagnon ambaye sasa atasajiliwa kwa mkataba wa miezi sita

MWANDISHI WA MICHEZO AFARIKI BAADA YA KURIPOTI FAINALI YA SIMBA NA AZAM

Picha
Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR MWANDISHI wa Habari za michezo wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Amina Athumani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Amina alikuwa visiwani Zanzibar kikazi, kuripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mwenyezi Mungu akamuongoza kuifanya kazi yake vizuri mwanzo hadi mwisho. Usiku wa kuamkia safari ya kurejea Dar es Salaam Jumamosi ndipo Amina aliyekuwa ana uja uzito wa miezi saba alipoanza kusumbuliwa kiafya Na inaelezwa asubuhi wakati anaelekea kwenye boti kurejea Dar es Salaam alianguka na kupelekwa hospitali binafsi, baadaye akahamishiwa Mnazi Mmoja. Siku hiyo hiyo Amina akajifungua mtoto ambaye kwa bahati mbaya alikwishafariki dunia.

Kispoti: YANGA NA MWAKA WA TAABU

Picha
Na Prince Hoza SIJUI nani aliyewadanganya Yanga SC kuachana na beki wake kiraka Mkongoman aliyenunua uraia wa Rwanda, Mbuyu Twite, alipokuwepo katika kikosi cha kwanza cha Yanga wala hakuwahi kuwaangusha Wanayanga. Chini ya Mbuyu Twite Yanga haikuwahi kufungwa magoli 4-0, chini ya Mbuyu Twite Yanga haikuwahi kupoteza mechi mbili mfululizo kwa kufungwa na timu za nyumbani, chini ya Mbuyu Twite Wanayanga waliziona jitihada zake. Jamaa huyo mwenye kifua kipana wakati mwingine aliamua kuibeba Yanga kupitia mikono yake, Twite ana nguvu za kurusha mipira hivyo aliweza kuisaidia Yanga kupata mabao kupitia mikono yake. Kwa hakika Mbuyu Twite alikuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho, Twite alishiriki kwenye kikosi cha mafanikio kilichotwaa mataji yote makubwa hapa nchini, Yanga ilitwaa ubingwa wa Bara mara mbilj mfululizo, ikatwaa kombe la FA, ikatwaa Ngao ya Hisani pia ikafuzu fainali za kombe la Shirikisho barani Afrika. Sidhani kama kuna mafanikio mengine zaidi ya hayo kwa soka l...

BURKINA FASO, CAMEROON SARE SARE MAUA AFCON, DIAMOND ACHIZISHA WATAZAMAJI

Picha
Burkina Faso imeilazimisha sare Cameroon ya kufungana mabao 1-1 katika mechi yao ya kwanza ya AFCON mjini Libreville nchini Gabon. Mechi hiyo ilionekana kama ya Cameroon ambao walitangulia kupata bao katika dakika ya 35 mfungaji akiwa ni Benjamin  Moukandjo na likadumu hadi mapumziko. Lakini Issoufou Dayo aliisawazishia Burkina Faso katika dakika ya 75 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare sare maua. Mwanamuziki wa miondoko ya kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Diamond Platinum alitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa michuano hiyo, Diamond aliwachizisha watazamaji na kuonekana wakimshangilia kwa kupiga makofi